Deliverance Church Zimmerman's Podcast
Religion & Spirituality:Christianity
Wakati Mungu Haajibiki | Rev. Beatrice Waithaka | DCIKZ
Msisitizo mwingi tumepewa wa kuweka tumaini letu kwa Roho Mtakatifu. Asubuhi ya leo nataka kutengeneza usawa. Bwana Mungu hatalitenda jambo lolote ambalo amekuwezesha kulitenda. Je unajua kwanba kuna wakati Mungu alimkemea Musa kwa sababu ya kumwomba? Kwanini? Kwa sababu kilicho takikana wakati ule sio maombi lakini ni matendo. Kutotenda ni nguvu ambazo zina uwezo wa kusimamisha mtiririko wa mwendo wa Mungu. (Inaction is a force that has the potential of stopping the flow and the move of God). Kutoka 14:15 Mwenyezi – Mungu akamwambia Musa, “Kwa nini mnanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele. Mkazo ni kwamba: “ Musa ni ya nini haya maombi ya kijinga na yasiyo ya lazima, unajua lakufanya, ninajua unapenda maombi, lakini huu sio wakati. Ni wakati wa kutenda. Mhubiri 3:1 Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake. Waambie waisraeli wasonge mbele, nyosha fimbo lako na kusema. Usifanye maombi kuwa njia ya kutoroka kwa ajili ya uwoga wa kuchukua hatua. Wapendwa maombi bila matendo yamekufa. Ukifanya kazi, itafanya kazi. Kukamata kubwa ni lazima uajibike kwa sehemu yako naye Mungu alikabidhi kwa sehemu yake. Mtume Paulo akasema katika 1 Wakorintho 9:24-25; Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu nayejinyakulia zawadi? Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji isiyoharibika. Kukimbia kwa njia ambayo itakupa tuzo. Mkimbiaji ambaye analenga macho yake kwa taji hahusiki na kasi ambayo wengine wanakimbia, bali anazingatia mbio zake. Labda wewe ni hatua moja tu kwa maisha tofauti, Mabadiliko katika kiwango, Mabadiliko ya hadithi yako, Mwanzo mpya, Wacha kuiahirisha. Je unaogopa nini? Sisi tumezaliwa na aina mbili tu za uoga;
• Hofu ya sauti kubwa
• Hofu ya kuanguka
Hofu zingine zote ni zile tumejifunza na tunaweza kutojifunza (unlearn). Ni wakati wa kugeuza ukurasa. Ni wakati wa kutenda mambo nje ya njia zako au mafikira yako. Ni wakati wa kutojiona duni. Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenya nguvu wauteka.
• Ni wakati wa kuanza kuchukua hatua. Mungu hangenyosha fimbo lake Musa, Mungu hangewanenea watu kwa niaba yake Musa
• Kijana unataka kufunga ndoa, Mungu hatamnenea yule mwana dada kwa niaba yako. Wacha kukonyeza (winking) macho gizani
• Mungu hatatuma vyeti vyako kwa huyo mkurugenzi
• Mungu hataandika hicho kitabu kwa niaba yako
• Mungu hatatengeneza muziki huo, endelea kuimba peke yako
• Hebu tusikizane miujiza yatendeka lakini sio jambo la busara kutegemea tu.
Create your
podcast in
minutes
It is Free