(Msimu wa 54: Kipindi cha 01)
Tunapoendelea na mfululizo wetu, “Nuru Halisi,” wiki hii, ninataka kukuuliza...unafikiri haki halisi ni nini?
Katika tamaduni zetu, watu wengi hufikiri na kuamini kwamba mema na mabaya ni suala la mtazamo, lakini Biblia inasema jambo tofauti kabisa. Mungu anatuambia kwamba kuna tofauti ya wazi kati ya mema na mabaya. Na tunaijua katika mioyo yetu. Katika Yeremia thelathini na moja (31), Mungu anatuambia, “Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.” Na hakika Yeye amefanya. Inaitwa dhamiri yetu. Tunajua tunapokosea na kufanya makosa.
Muujiza wa kweli ni kwamba Mungu wetu mkamilifu, mtakatifu, mwenye haki hutupatia msamaha wa makosa yetu kwa kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wetu. Na kisha, anatupa moyo mpya wa imani na utii. Sisi ni wenye haki kupitia Yesu. Je, unaweza kushiriki na nani Habari hii njema leo?
Kwa nyenzo za kukusaidia kushiriki imani yako, tembelea tovuti yetu katika sharelifeafrica.org.
___________________________________
ShareLifeAfrica ni redio ya Kikristo na kipindi cha podikasti cha Evangelism Explosion International Africa Ministry; ambayo imejitolea kukupa zana na nyenzo zinazohitajika ili kushiriki imani yako na wengine kwa ujasiri na kwa ufanisi.”
Create your
podcast in
minutes
It is Free